“Mambo 13 Vijana Wanayodai Ni Sababu ya Umasikini, Lakini Ukweli Ni Visingizio Tu”*
1. “Nimetoka familia maskini”
👉 Kile unachofikiria:
Unaamini background yako imeamua mwisho wako.
👉 Ukweli:
Familia yako imekupa mwanzo, si mwisho. Watu wengi waliofanikiwa hawakutoka kwenye maisha mazuri.
👉 Mfano:
Kijana anayelalamika hana support ya familia anaweza kuanza kuuza vitu vidogo mtandaoni au mtaani. Taratibu anajijenga.
👉 Ujumbe:
Usitumie historia kama kisingizio itumie kama motivation.
2. “Sina connection (watu wa kunisaidia)”
👉 Kile unachofikiria:
Unaamini lazima uwe na mtu mkubwa nyuma yako ili ufanikiwe.
👉 Ukweli:
Connection zinajengwa, hazizaliwi nazo.
👉 Ujumbe:
Anza kujionyesha, dunia itaanza kukutambua.
3. “Sina elimu kubwa”
👉 Kile unachofikiria:
Unafikiri bila degree huwezi kufika mbali. Ukiona watu wenye degree na elimu nyingine kubwa na wana maisha mazuri Unajilinganisha na umasikini wako kuwa ni sehemu ya chanzo.
👉 Ukweli:
Elimu ya darasani ni sehemu tu ujuzi (skills) ndiyo inalipa zaidi.
👉 Ujumbe:
Jifunze skill, sio tu vyeti.
4. “Nimekosa ajira”
👉 Kile unachofikiria:
Unaona maisha yamesimama kwa sababu hujaajiriwa. Umesoma lakin elimu yako haikukufisha kwenye ajira, unakumbwa umasikini na hali ngumu ya maisha.
👉 Ukweli:
Ajira ni njia moja tu sio mwisho wa maisha.
👉Badala ya kusubiri ajira, unaweza kuanza biashara ndogo: kuuza bidhaa, kufanya freelancing, au content creation.
👉 Ujumbe:
Usisubiri kuajiriwa jiajiri.
5. “Wengine wanafanikiwa kwa rushwa”
👉 Kile unachofikiria:
Unaona mafanikio ya watu si halali, hivyo unakata tamaa.
Unamuona mwanamke mzuri kwenye ajira fulani nyeti, fikra inakutuma kuwa amefika hapo kwa rushwa ya ngono.
👉 Ukweli:
Ndiyo, kuna wanaofanikiwa kwa njia mbaya lakini wengi wanafanikiwa kwa juhudi.
👉 Mfano:
Content creators wengi wamejenga majina yao bila shortcut yoyote.
👉 Ujumbe:
Focus na njia yako, sio shortcuts za wengine.
6. “Watu watanionaje”
👉 Kile unachofikiria:
Unaogopa kuanza kitu kwa sababu ya maoni ya watu. Unaogopa kuzungusha karanga na andazi ukiogopa kuhusu juu ya elimu yako, nafasi uliyo nayo kwa watu wako.
👉 Ukweli:
Watu watakuongelea hata usipofanya kitu.
👉 Ujumbe:
Usiishi maisha kwa approval ya watu.
7. “Nitasubiri opportunity kubwa”
👉 Kile unachofikiria:
Unangoja nafasi “perfect”.
👉 Ukweli:
Fursa kubwa huanza kama kitu kidogo sana.
👉 Mfano:
Ukianza kuuza bidhaa moja leo, inaweza kuwa biashara kubwa kesho.
👉 Ujumbe:
Anza na kidogo, ndipo ukubwa huanzia.
8. “Nimejaribu mara moja nikashindwa”
👉 Kile unachofikiria:
Unaona failure moja ni mwisho.
👉 Ukweli:
Watu waliofanikiwa walishindwa mara nyingi kabla ya kushinda.
👉 Ujumbe:
Failure si mwisho ni somo.
9. “Sina muda”
👉 Kile unachofikiria:
Unaamini uko busy sana kuanza kitu kipya.
👉 Ukweli:
Kila mtu ana saa 24 tofauti ni matumizi ya muda.
👉 Mfano:
Masaa unayotumia scrolling mtandaoni unaweza kuyatumia kujifunza au kuanza biashara.
👉 Ujumbe:
Tatizo si muda ni vipaumbele.
10. “Biashara ni ngumu sana”
👉 Kile unachofikiria:
Unaogopa kuanza kwa sababu ya changamoto.
👉 Ukweli:
Kila kitu kigumu mwanzoni hata maisha yenyewe ni magumu.
👉 Mfano:
Ukianza biashara leo, utafanya makosa lakini hapo ndipo unajifunza.
👉 Ujumbe:
Ugumu ni sehemu ya safari, sio sababu ya kuacha.
11. “Soko limejaa sana”
👉 Kile unachofikiria:
Unaona huwezi kuingia kwenye biashara fulani kwa sababu watu ni wengi.
👉 Ukweli:
Soko halijai linahitaji watu tofauti.
👉 Mfano:
Watu wengi wanauza nguo, lakini anayetoa huduma nzuri na ubunifu anashinda.
👉 Ujumbe:
Tofauti yako ndiyo faida yako.
12. “Nina majukumu mengi”
👉 Kile unachofikiria:
Unaona majukumu yanakuzuia kufanikiwa.
👉 Ukweli:
Watu wengi waliofanikiwa walikuwa na majukumu makubwa zaidi.
👉 Mfano:
Mtu anaweza kusoma, kufanya kazi ndogo, na bado kujenga kitu chake pembeni.
👉 Ujumbe:
Majukumu si kizuizi ni sababu ya kusonga mbele.
13. “Nitasubiri hali iwe nzuri”
👉 Kile unachofikiria:
Unaona lazima kila kitu kiwe sawa kwanza.
👉 Ukweli:
Hakuna siku hali itakuwa perfect.
👉 Mfano:
Ukisubiri pesa, muda, au mazingira mazuri utaishia kusubiri maisha yote.
👉 Ujumbe:
Anza na ulicho nacho, ulipo.
By
Taufiq abdallah siraji
Mwandishi nguli wa vitabu. 0713 308 647
Tuachie comment hapo
ReplyDelete