✍️Katika maisha yako kama mwanaume, usije ukamdharau mwanaume mwenzako kwa sababu tu leo wewe unaonekana upo juu kuliko yeye.
✍️Kumbuka maisha hayasimami sehemu moja. Leo unaweza kuwa na kazi nzuri, biashara inayoenda, pesa mfukoni na watu wanakuheshimu. Lakini kesho upepo unaweza kubadilika bila hata onyo.
✍️Usimcheke mtu kwa sababu hana kazi, hana pesa, au maisha yake hayapo sawa kwa sasa. Hujui anapitia nini, hujui anapigana vita gani kimya kimya. Wakati mwingine yule unayemdharau leo, kesho anaweza kuwa juu yako.
✍️Na pia usiwe mtu wa majivuno kwa kile ulicho nacho kwa wakati huo. Majivuno yanapoteza heshima yako taratibu. Watu wanaweza kukuchekea mbele yako, lakini mioyoni mwao wanakutazama kwa dharau.
✍️Mali, vyeo, umaarufu na nafasi ulizonazo si vitu vya kudumu. Ni kama msimu vinaweza kuja na vinaweza kuondoka. Leo una gari, kesho unaweza kutembea kwa miguu. Leo unaitwa “boss”, kesho unaweza kuwa unatafuta hata mtu wa kukusaidia.
✍️Kilicho cha kudumu ni tabia yako, unyenyekevu wako, na namna unavyowatendea wengine.
✍️Heshimu watu ukiwa juu, ili kesho ukishuka upate wa kukunyanyua.
Kuwa mnyenyekevu ukiwa na kila kitu, kwa sababu maisha yana mzunguko.
✍️Uanaume wa kweli sio kumdharau mwingine, bali ni kuinua mwingine hata pale unapokuwa juu kuliko yeye.
Usisahau kuacha comment yako.
No comments:
Post a Comment